ZAIDI
ya wasichana 160 wa jamii ya
wafugaji wa kabila la Kimasai wamenusurika kufanyiwa mila ya ukeketaji na
badala yake wamefanyiwa tohara mbadala .
Wasichana hao waishio katika
kata ya Kang'ata iliyoko wilayani Handeni wameweza kunusurika kufanyiwa
mila hiyo kufuatia elimu waliyoipata kupitia mradi wa Kijana wa leo
unatekelezwa na shirika la Amref
Akizungumza wakati wa sherehe
za kuvuka rika kwa jamii hiyo meneja mradi huo Dar Aisha Byanaku alisema kuwa
kufuatia elimu kuhusu madhara ya ukeketaji waliyotoa katika eneo hilo
wamefanikiwa kuwa komboa wasichana hao.
"Lengo la mradi kuhakikisha
tunawakomboa wasichana wa jamii ya wafugaji na wanaishi pembezoni
kuachana na mila potofu ambazo zina madhara kwa walengwa"alisema Dkt
Byanaku.
Alisema kuwa mradi huo unatekelezwa
kwa kipindi cha miaka mitatu katika wilaya hiyo umelenga kuwa komboa
wasichana 500,lakini kwa mwaka mmoja pekee wameweza kufanikiwa kuokoka
wasichana 170 kufanyiwa vitendo vya ukeketaji.
Hata hivyo Kaimu mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Handeni Noeli Abel alisema mimba za
utotoni pamoja na ukosefu wa taarifa sahihi za elimu ya ujinsia kwa vijana ni
sehemu ya changamoto kubwa zinazowakabili vijana wa kitanzania
kwa sasa.
Alisema changamoto hizo
zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha vijana wengi kushindwa kufikia
malengo ya kimaendeleo waliyojiwekea kwa wakati ,na wengine huishia
kukatiza ndoto hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni