WAZIRI
wa
afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya
kikazi Wilaya ya Pangani kuona
changamoto zinazo wakabili wananchi katika hospital ya Wilaya hiyo na kuahidi
kuwapatia mashine ya XRAY nyingine ya
kisasa .
Akizungumzia kituo cha afya mwera Mwalimu ameahidi
kuhakikisha kituo cha afya cha mwera kinakamilika kwa kujengwa chumba cha
upasuaji cha kisasa na kujengwa wodi moja na nyumba moja ya mtumishi pamoja na
maabara ya damu kupitia mradi wa benk ya dunia kwa mwaka wa 2017/ 2018 kwa sera
ya kila halmashauri kujengewa kituo cha afya.
Pia mwalimu amesema atahakikisha hospital inapata
watumishi wa kutosha pae serikari itakapo anza kuajili na kuleta kifaa cha kupimia saratani ya shingo ya
kizazi.
Katika ziara hiyo waziri wa afya maendeleo ya jamii
jinsia wazee na watoto amechangia mifuko ya cement 100 kwa ajili ya ukarabati
wa zahanati ya kigurusimba iliyopo wilayani Pangani.
Kwa upande wa maendeleo ya jamii ameahidi atahakikisha
kupitia mfuko wa (WDF) atasaidia sh mil 12 kwa ajili ya vikundi vya kina mama
naatashirikisha serikali kupitia UNFPA kujenga kituo maalumu cha dawati la jinsi
.
Aidha waziri ameipongeza idara ya afya Wilaya ya Pangani
kwa kuongoza mkoa wa Tanga na kuwa tatu bora
Tanzania kwa kusajili wanachama wa CHF kwa asilimia kwa asilimia 72%.
Mwalimu amepongeza pia huduma zinazotolewa kwa wazee
katika hospitali ya wilaya pamoja na kuwapatia vitambulisho wazee 67% na
asilimia 975 ya upatikanaji wa dawa muhimu pamoja na kupambana na vifo vya
wakina mama wajawazito kwa asilimia 0% kwa mwaka huu.
Waziri Mwalimu ameahidi kushirikiana na uongozi wa
Wilaya ya Pangani kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwataka viongozi wa wilaya
hiyo kuweka kipaumbe zaidi katika swala la elimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni