Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakiangalia gari ambayo
ilikamatwa Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ikiwa na wahamiaji haramu wapatao
150 ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia ambao walikamatwa
wakati wakiwa wapo safari kuelekea mikoa ya kusini.
HABARI.
Matukio ya namna hiyo
katika Mkoa wa Pwani yanaonekana kumsikitisha na kumlazimu Waziri
wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati sakata hilo kwa kutangaza
rasmi kupambana vilivyo na watu wote ambao watabainika wanajihusisha na vitendo
hivyo vya mauaji ili waweze kukamatwa haraka na kuweza kufikishwa katika
vyombo vya dola ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Waziri nchemba ametoa agizo
hilo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea askari polisi, magereza, uhamiaji
pamoja zimamoto wa Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweza kukagua shuguli mbali mbali
za utekelezaji ya majukumu yao ya kila siku ikiwemo na kuweza
kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na kuweka mikakati
kwa ajili ya kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
“Kumekuwepo katika baadhi ya
maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna baadhi ya viongozi wa vijiji pamoja na wakulima na
wafugaji kupoteza maisha, kwa hili sisi kama Wizara hatuwezi kulivumilia hata
kidogo kwani kwa sasa tumejipanga ii kuweza kuwabaini watu ambao wanahusika
katika vitendo hivyo,”alisema Waziri.
Alisema kuwa anasikitishwa
kuona mauaji yanafanyika kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu
za nchi, kwa mwananchi yoyote kuamua kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya
vitendo vya mauaji hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo na wale wote
watakaobainika wataweza kuchukuiwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
Aidha Waziri Nchemba alibainisha
kuwa kutokana na kuwepo kwa wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini bila
ya kuwa na vibali Wizara yake imeweka mikakati kabambe ya kuongeza doria usiku
na mchana katika sehemu mbali mbali ikiwemo mipaka, fukwe za bahari
pamoja na bandari bubu amabzo zimekuwa zikitumika kuwapitisha raia hao wa
kigeni.
“Tatizo lawahamiaji haramu katika
Mkoa wa Pwani bado ni tatizo kubwa kwani imekuwa ndio kama lango la kuingilia
pindi wanapokuja hasa katika maeneo ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na
Wilaya ya Kibaha, hivyo sisi katika hili tumeshajipanga ili kuweza kuthibiti
njia zote ambazo wamekuwa wakizitumia katika kupita,”alisema Nchemba.
Pia katika hatua nyingine Nchemba
alitoa wito kwa wananchi wote kushirikiana bega kwa began a serikali pamoja na
vyombo vya dola katika kuwabaini na kuwafichua watu ambao wanakuwa na
mashaka nao kwani wengine wanaingia nchini kwa ajili ya kufanya matukio mbali
mbali ya uharifu wa kutumia silaha.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Mjini Silvestry Koka ameiomba serikali ya awamu ya tano kupitia .
Wizara ya mambo ya ndani
kuhakikisha inaongeza vitendea kazi pamoja na kuongeza ujenzi wa vituo
vingine vidogo vya polisi ambavyo vitaweza kusaidia kuimarisha hali
ya ulinzi na usalama pamoja na kupamba na waharifu ambao wanaingia Mkoa wa
Pwani kinyemela na kujificha.
Pia Koka alimwomba waziri wa mambo
ya ndani kuweka utaratibu wa kuhakikisha vituo vidogo vya polisi vilivyojengwa
vinakuwa wazi wakati wote lengo ikiwa ni kuweza kupambana na matukio mbali
mbali ya uharifu ambayo yanakuwa yanajitokeza bila ya kuwa na muda
maalumu hivyo vituo vikiwa wazi kutaweza kusaidia kupunguza hali ya uharifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni