Jeshi la polisi mkowa wa Tanga
limefanikiwa kukamata silaha mbili aina ya SMG na risasi 23, Bastola 1 risasi 1
Kisu na Majambia viliyotumika katika mauwaji yaliyofanyika mei 31 mwaka huu
kata ya Kibatini Amboni mkoani Tanga.
Akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake laeo, Kamanda
wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, alisema kukamatwa kwa vifaa hivyo ni ushirikiano na vyombo vya usalama na wananchi.
Kamanda wa polisi mkoa Tanga Leonard
Poul alisema walifanikiwa kuwakamata watu watatu walioshiriki kwenye mauwaji ya
kikatili ya kibatini na kuwataja majina ya wahalifu kuawa ni Abdukalimu
Singano, Sefu Jumanne na Ramadhani Muhamedi ambao wote walifariki baada ya
kujaribu kukimbia eneo la msituni wa kibatini mara baada ya kuonyesha
walipokuwa wamefukia silaha.
Kamanda Poul alisema kwa sasa
mapango ya amboni ni salama na hayana tena matishio ya majambazi na kuwataka
wananchi kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote.
Kamanda alisema “hawa ndiyo waliuwa watu 8 kwa kuchinjwa kikatili na matukio ya kuuwawa
watu katika maduka makubwa na vituo vya mafuta na uporaji, polisi walikuwa katika msako mkali
na leo hii niseme Mapango ya Amboni ni Salama” alisema Poul.
Pia kamanda wa polisi mkoa wa Tanga
amewataka wananchi na wakazi wa mkoa wa Tanga kutoa taarifa pindi wanapoona mtu
wasiye mwelewa watoe taarifa kwa jeshi la polisi au kituo kilicho karibu
nao.
Nahivi ni baadhi ya vyombo walivyokuwa wanatumia kwenye mapango ambavyo jeshi la polisi wameweza kuvishikilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni