MAMLAKA ya
Majisafi na usafi wa mazingira jiji la Tanga imekabidhi madawati 40 kwa ajili
ya uchangiaji wa kampeni ya kutoa elimu bora kwa watoto wa shule za jiji la
Tanga ili kutimiza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Pombe Magufuri.
Akizungumza wakati wa makabidhiano katika shule ya Jaje kata
ya Tanga sisi Mkurugenzi Mtendaji Tanga Uwasa Eng. Joshua Mgeyekwa amesema madawati
haya yenye thamani ya shilingi mil 3 ni sehemu ya kuwaunga mkono wateja wao wa Tanga Uwasa katika kuboresha
mazingira ya kusomea watoto wao wanaosoma shule ya msingi jajae kuondokana na changemoto
ya kukaa chini.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa amesema shule hii
inayo changamoto ya mashimo ya choo na kuhaidi kutatua changamoto hiyo
kuhakikisha walimu pamoja na wanafunzi wanafurahia mazingira yaliyopo shuleni.
Eng. Mgeyekwa amesema mamlaka Majisafi na usafi wa mazingira iko
tayari kuunga mkono shughuli zote zenye kuleta maendeleo katika Wilayani na Mkoani
wa Tanga.
Akipokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdull
Lutavi amewasii wanafunzi kuyatunza madawati hayo ili yaweze kutumika kwa
vizazi hata vizazi.
Katika makabidhiano hayo ambayo yalifanyika katika shule
ya Jaje Mkuu wa Wilaya alipokea madawati sabini arubaini kutoka Tanga Uwasa na
mengine therathini kutoka kwa wadau wengine waliojitolea kuunga mkono agizo
hili la Rais.
Naye Afisa Elimu Kata ya Duga Jani Lyatuu ameshukuru
zoezi hili lililoanzwa na Mamlaka Majisafi na usafi wa mazingira kwa shule ya msingi Jaje na kusema kwa sasa
kata hii ya Duga ina mapungufu ya
madawati (628) kwa shule zote nne za kata hiyo na kuwaomba wadau mbalimbali
kujitokeza kama walivyofanya Tanga Uwasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni