Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kukamata bunduki ya kivita aina ya AK47 iliyokuwa na risasi 37 .
Akionyesha silaha
hiyo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa
Polisi Mkoa Tanga, Leonard Poul, alisema katika ukaguzi wa magari kizuizi cha
Chekelezi Wilayani Korogwe na mtu anaedhaniwa kuwa Jambazi aliefahamika
kwa jina la Benjamin Wales alikuwa amebebe silaha hiyo
katika begi akisafiri kutoka Karatu kuelekea Dar es Salaam.
Jambazi hilo liliuwawa na polisi wakati aliporuka kwenye
gari kujaribu kuwatoroka.
Jeshi la polisi Mkoani Tanga limeongeza ulinzi na operesheni
kukabiliana na watumiaji silaha bila kibali ,uhalifu, upitishaji wa wahamiaji
haramu na bidhaa za magendo.
Jeshi hilo limefanikiwa kukamata silaha na watuhumiwa wa
uhalifu wa matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani.
Pia kamanda amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa
wa Tanga kutoa taarifa za kufichua vitendo viovu katika jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni