Ijumaa, 10 Juni 2016

WAKAZI WA TANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA.BOMBA LA MAFUTA



MAMLAKA ya bandari mkoani Tanga imewataka wakazi wa mkoani Tanga na maeneo ya jirani na bomba  la mafuta litakapopitia  kuchangamkia fursa za maendelea na kujianda vizuri na mradi wa bomba hilo litokalo Uganda hadi Tanga Tanzania.
Hayo yalisemwa na Afisa Habari wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga Moni J. Msemo katika maonyesho ya kimataifa yaliyofanyika  Mkoani Tanga katika viwanja va mwaako.

Moni aliwataka wananchi na wakazi wa Mikoa ambayo Bomba hilo la mafuta litakapopita kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya ajira mbalimbali zitakazo tokea kwa Watanzania waliopo katika maeneo ya jirani na mradi huu.

Pia aliwataka watanzania na wakazi wa Mkoa wa Tanga kuhusubiri mradi huu kiujuzi kwa kuingia vyuo mbalimbali ili kujipatia mafunzo yatakayo wasaidia kupata ajira kwenye mradi huo.
“Moni alisema, mradi huu mkubwa utatoa ajira za ufundi uendeshaji vyombo mbalimbali vya mradi, lakini fursa hii itagusa watu wote Mkoani Tanga ikiwa ni pamoja na Mama ntilie, Wenye Hotel hata wauzaji Vyakula pamoja na Wakulima” alisema moni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni