Jumatano, 15 Juni 2016

ZAIDI YA WATEJA 70 WANAOISHI KANGE KASERA MKOANI TANGA WAUNGANISHWA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA.



MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Tanga UWASA) imeongeza
wingi wa maji kwa kuchimba kisima kimoja kirefu katika kitongoji cha
Mwakileo ambacho kina uwezo a kuzalisha Lita 5,000 za ujazo kwa siku.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Joshua Mgeyekwa amebainisha hayo
jana katika mahojiano na mwandishi wetu kuhusu huduma mpya na namna
wanavyopanua mtandao wa huduma zake ili kuhakikisha zinawafikia walaji
hasa katika maeneo mapya ya miji na ujenzi wa viwanda.

Alisema katika siku za hivi karibuni Tanga Uwasa imebadilisha dira
yake na kuwa Mamlaka inayomjali mteja ambapo pamoja na mambo mengine
inahakikisha inafuata viwango vya ubora vinavyohitajika kimataifa
katika kuwahudumia wateja ikiwemo kutoa Ankara kulingana na matumizi
ya mteja.

“Tumeongoza wingi wa maji safi kwa kuchimba kisima kimoja kirefu
katika eneo la  Mwakileo na tayari tumelaza bomba kubwa kutoka katika
chanzo chetu kikuu kilichopo Pande ili kujaza maji katika tangi
lililoko Kwambogo kabla ya kusambza kwa wateja wetu walioko kwenye
maeneo mbalimbali ya mabokweni na Kasera”, alisema na kuongeza.

 “Njia hii mpya ya bomba imesaidia kupunguza kiasi cha maji kilichokuwa
kinapotea kutokana na bomba la awali kulazimika kuungwa ungwa njiani
kabla ya kufika kwenye Tangi hivyo wigo wa huduma sasa umepanuka
ikilinganishwa na awali na wataeja tayari wateja wapya zaidi ya 70
wanaoishi maeneo ya Kange Kasera wameunganishwa,”.

Mgeyekwa akifafanua zaidi kuhusu namna Mamlaka inavyowanavyojali
wateja alisema kuanzia mwezi Julai mwaka huu wakazi wa Tanga watalipia
nkara zao za maji kwa kutumia mitandao ya simu za mkononi.

“Tunaanzisha ulipaji Ankara za maji kwa kupitia mifumo ya M-pesa na
Tigopesa pamoja na benki ya CRDB ambayo tuliitumia tangu miaka mitatu
iliyopita hata taarifa za wateja kuhusu kiasi gani cha Ankara,
anatakiwa kulipa tutawatumia kwa simu zao za mkononi …Lengo letu ni
kuhakikisha tunafunga vituo vyote vya malipo ili watu wasipoteze muda
kupanga foleni badala yake muda huo wakautumia kufanya shughuli
nyingine za kujiongezea kipato, “alisema.

Aidha, alisema kwa sasa mamlaka inaendelea kuwaelimisha wateja wake
kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo haki na wajibu wao pamoja na
kuwasikiliza ili kujua changamoto zao hatimaye zipatiwe ufumbuzi wa
haraka.

Alisema lengo kuu la kuwaelimisha ni ili kuwajengea uwezo na kuongeza
msisitizo katika kuwahimiza kushiriki kulinda hifadhi ya vyanzo vya
maji ili gharama za huduma zisipande sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni