Jumapili, 21 Mei 2017

WATOTO WAWILI WA FAMILIA MOJA WAFA MAJI WILAYANI MKINGA MKOANI TANGA.


JESHI la Polisi mkoani Tanga limewataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki cha mvua ambapo Madimbwi mashimo pamoja na mito iliyojaa maji.

Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba alipotembela katika kitongoji cha mwakamba kata ya Moa wilayani Mkinga, ambapo watoto wawili wa familia moja Mwanasha Omary mwenye umri wa miaka (9) na Omary Mwazizi miaka (5)wamekufa maji baada ya kutumbukia kwenye Dimbwi tarehe 20/5/2017 majira ya saa 2:45 asubuhi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda Wakulyamba amesema watoto hao walitumbukia katika shimo lililokuwa likichimbwa mchanga kwa ajili ya ujenzi na mtoto Omary Mwazizi ndiye alianza kutumbukia na dada yake mwanasha akajaribu kumuokoa naye akatumukia na kuzama.

Kamanda wakulyamba amewataka viongozi wa Serikali wote kukagua na kubaini maeneo hatarishi kama vile madimbwi mashimo na mikondo ya maji na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuyafukia au kuweka alama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni