Mamlaka ya Chakula na madawa (TFDA) imewataka wananchi
kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa kwa nyakati tofauti kwenye
mitandao ya kijamii kuwa kuna soda aina ya ‘Novida’ kutoka nchini Nigeria
zimeingizwa nchini kinyemela na zina sumu ya virusi vya Ebola na tayari
zimesababisha vifo vya watu 180 nchini humo.
Taarifa ya Mamlaka hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki
iliyopita ikiwa ni mwendelezo wa taarifa yake ya awali iliyotolewa mwezi Aprili
2017 inabainisha kuwa taarifa zinazosambazwa za kuingizwa soda zenye sumu ya
Ebola haina ukweli na inapaswa kupuuzwa.
Kwenye taarifa hiyo, TFDA imeeleza kuwa inatambua uwepo wa
soda ziitwazo Schweppes Novida zinazozalishwa na viwanda vya Coca-Cola
Kwanza,Bonite na Nyanza Bottlers na soda hizo zinazalishwa kwa kuzingatia
mifumo bora ya uzalishaji na zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.
‘’Kama ilivyo kwa bidhaa nyingize za
chakula,vipodozi,vifaa vya tiba na vitendashi,soda za Schweppes Novida
ambazo zimesajiliwa na TFDA zimekuwa zikifuatiliwa katika soko kupitia mifumo
liyopo ya udhibiti ili kujiridhisha kuwa zinaendelea kukidhi vigezo vya usalama
na ubora kwa lengo la kulinda afya ya mlaji’’inabainisha sehemu ya taarifa ya
TFDA .
Soda aina ya Schweppes Novida kwa hapa nchini
ilizinduliwa mwaka 2013, inatengenezwa na kusambazwa na viwanda vya Coca-Cola
vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Kilimanjaro.Soda hizi
zinazopendwa na wateja zinatengenezwa kwa ujazo wa ml 300 na ml 500 zipo za aina
ya Mandarin Cooler zenye ladha murua ya machenza na Pineapple Breeze zenye
ladha ya Nanasi.
Cheap cheap prices of titanium, the world's hottest new oil
JibuFutaCheap, reliable, solo titanium razor affordable platinum-carbon steel for your car. babyliss nano titanium flat iron Shop our great deals now for ti89 titanium calculators the babyliss pro nano titanium straightener most popular models. sugarboo extra long digital titanium styler