Jumatano, 3 Mei 2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, TANGA PRESS CLUB YAHAMASISHA UCHANGIAJI DAMU KWA WAANDISHI NA WADAU..

Katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba akishiriki uchangiaji wa damu salama,akitolewa damu na  Daktari Stivin Mnyawoga kutoka  hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga  kitengo cha maabara, ,  zoezi la hiari lakuchangia damu lililoratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Tanga (Tanga Press Club TPC) 

Mwandishi wa Habari wa Radio Nnuor ya Tanga Ally Zumo akichangia damu kwa hiari  katika zoezi lililofanyika  eneo la Tanga Press Clabu.



Daktari kutoka maabara  hospitali ya Bombo Tanga, Hamis  Kayoga, akimtoa damu Sadik Shembilu wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama liliratibiwa na Clabu ya Waandishi wa Habari Tanga ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Mwandishi wa  Tanga one blog Pamela Chaula akitoa damu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari inayoadhimishwa leo Duniani kote.
Daktari wa hospitali ya Bombo Tanga, Fransisi Julias  kitengo cha maabara, akimtoa damu, Abdalla Yussuf mkazi wa Mikanjuni wakati wa zoezi la uchangiaji wa damu salama liliratibiwa na Clabu ya Waandishi wa Habari wa Tanga






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni