Jumanne, 17 Januari 2017

SERIKALI YAWARUHUSU WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUTUMIA MIHURI YAO.



BAADA ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.

''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema

Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.

Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi.

MEYA WA JIJI LA TANGA MUSTAPHA SELEBOSE NA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA WAKIZIMA SITOFAHAMU ILIYOJITOKEZA KATI YA ASKARI WAJIJI NA WAMILIKI WA MABASIYA MOMBASA.






Meya wa Jiji la Tanga Alhaj Mustaph Selebose akiwa na Mbunge wa Tanga Mussa Mbaruku akizungumza na wasafirishaji wa mabasi yaendayo Mombasa baada ya kutokea kutoelewana kati ya Askari wa Jiji na wamiliki wa Mabasi hayo
  
HABARI
ASKARI wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na
kumlazimu Mbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasi na Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingilwa  na wafanyabiashara hao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.


Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu
na Assad Hotel ambapo kulikuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata
moja ya gari linaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kutoa faini.

Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge Mussa Mbaruku ambaye yupo mkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoani Dodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio na kuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisi zao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.

Akizungumza  na wasafirishaji hao,Mbunge Mbaruku aliwataka kuwa watulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzi kutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketi hivi
karibuni mjini hapa.

Aidha Mbunge Mbaruku alishtushwa na kitendo cha askari hao
kuchukua ushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambaye alisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo na wanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zote ambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.

Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo
na atakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine za kielektroniki.

Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za
Tanga Mombasa Mohammed Nassor alisema swala lilowashtua zaidi ni kutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jambo ambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Selebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs na hawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashine hizo.

Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari na kulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu za
kutozwa faini kwa mfumo wa mashine.

Jumatatu, 16 Januari 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASEMA TANZANIA HAMNA NJAA ATOA SABABU YA KUPANDA KWA BEI YA MAZAO.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania kutosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la  kupandisha bei za vyakula.

Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Dodoma baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.

“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.

Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.

Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake.
Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Alhamisi, 12 Januari 2017

SERIKALI HAINA CHAKULA CHA MSAADA ASEMA RAIS MAGUFULI..



RAIS John Magufuli amesema inawezekana asiwe mwanasiasa mzuri, lakini siku moja atakumbukwa kwa mambo ambayo anayafanya, kwa sababu dhamira yake ni nzuri katika kusimamia ubadhirifu wa fedha za umma na kusimamia miradi ya maendeleo ili watanzania wote wanufaike.

Pia amesisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi. Aidha, katika kusimamia kauli zake mkoani Simiyu, Rais Magufuli ameagiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu ambayo aliweka jiwe la msingi, ujenzi wake jana kujengwa kwa Sh bilioni 10 na kukataa kiwango kilichokuwa kimekadiriwa cha Sh bilioni 46.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Somanda wilayani Bariadi, kabla ya kwenda kuzindua ujenzi wa barabara.

Awali Rais alikuwa na mikutano mingine katika vijiji vya Nyashimo, Masanzakona, Lamadi na Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Nimeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali, ujenzi wake wamesema ni Shilingi bilioni 46, nimesema kitu hicho hakiwezekani, tena wamekosea sana kuniita mimi kuja kuweka jiwe la msingi,” alisema Rais Magufuli.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), Rais Magufuli alikataa gharama alizoelezwa, kwa maelezo kuwa ni kubwa.

“Haiwezekani pale Chuo Kikuu Dar es Salaam majengo yote yale yalijengwa kwa Sh bilioni 10, hapa jengo moja Sh bilioni 46, haiwezekani hata kidogo, nitaleta shilingi bilioni 10 kutoka ndani ya Serikali na hospitali hiyo ikamilike,” alisema.

Rais Magufuli alisema amekaa katika sekta ya ujenzi kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo alisema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ina majengo 20 yenye ghorofa nne ambazo zilijengwa kwa Sh bilioni 10.

“Mkitaka mkalete majengo yale ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbandike hapo, mtajua, nyie jengo hilo moja tena la ajabu ajabu, mnasema bilioni zote hizo, haiwezekani na siku ya kuzindua nitakuja mimi,” alisema.

Rais Magufuli alisema fedha za ujenzi wa barabara hiyo zote, zimetolewa na Serikali ambapo alimuagiza Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kilometa 48.9 zilizobaki katika barabara hiyo ndani ya wiki moja, ziwe zimetangazwa kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.

Alisema kwa kujengwa barabara hiyo, wananchi wa mkoa huo wataweza kufanya biashara kwa urahisi, ambapo amewaomba wananchi kuitumia vizuri barabara hiyo na kuilinda.

“Imekuwa ni kawaida barabara ikijengwa inakuwa chanzo cha ajali, watu wanaendesha kwa fujo, badala ya barabara kuwatunza inakuwa ndio chanzo cha mauaji, natoa mwito tuzingatie sheria za barabarani nisije kusikia baada ya siku chache imeua,” alisema.

Rais Magufuli aliwataka wananchi ambao wako ndani ya mita 2.5 kila upande, eneo ambalo barabara hiyo itapita, waanze kuondoka, wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mradi huo.

Rais alisema pia kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa, wanadai kuwa kuna njaa nchini, ambapo alisema kuwa kama kuna njaa, ni yeye atatoa tamko hilo.

“Wapo wafanyabiashara wachache waliokuwa wamezoea panatokea ukame kidogo, wanatumia vyombo vya habari vichache na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, lengo lao wasamehewe kodi,” alisema.
Alisema wafanyabiashara hao, wameleta mahindi yaliyo katika ubora usiofaa kwa lengo la kuuza bila kulipa kodi ili wapate faida.

“Yupo mfanyabiashara mmoja ameleta tani 25,000 za mahindi, anataka tumsamehe kodi, tumeshamkata kodi na huo ndio mchezo wao, wanawaambia andikeni kuna njaa, anayejua kuna njaa ni Rais,” alisema Rais Magufuli.
Alisema wabunge mwaka jana wakiwa katika vikao vya Bunge, walisema chakula ni kingi na kushauri kiuzwe nchini Uganda, lakini sasa hivi wanadai kuwa chakula hakitoshi.

Hivi karibuni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto, aliitaka Serikali itangaze rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria.

Zitto alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia ACT-Wazalendo, ambapo alisema bei ya chakula inazidi kupanda kutokana na uhaba wa chakula.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi hata kidogo, na kueleza kuwa jukumu la serikali siyo kugawa chakula cha bure kwa wananchi.

Alisema kuwa serikali haiwezi kutoa chakula cha msaada kwa watanzania zaidi ya milioni 50 nchi nzima, huku akiwataka wananchi kutowasikiliza wanasiasa ambao wanafanya siasa za kizamani.

“Jukumu la Serikali sio kuleta chakula kwa sababu serikali haina shamba la kulima, ni lazima niwaambie ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli, na wanasema asiyefanya kazi na asile…. maana yake na asipokula si afe, niwaombe mfanye kazi,” alisema Rais Magufuli.

Alibainisha kuwa kazi kubwa ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za fya, barabara, maji, umeme pamoja na elimu, na siyo kutoa chakula cha bure.

Rais alisema kuna maeneo hapa nchini, ambayo mvua zimenyesha na hazikutosha, hivyo wananchi wajipange kulima mazao ambayo hayatahitaji maji mengi na pia kuchukua muda mrefu kabla ya kuvunwa na sio kwamba kuna njaa.

“Ninafahamu wapo wanasiasa wachache ambao wanafikiri mzee bure hajatoka kichwani kwao, kila kitu kikitokea serikali ifanye, serikali ninayoiongoza mimi haitatoa kitu, mlinichagua niwaeleze ukweli na mimi nawaeleza ukweli,” alisema Magufuli.

Aliongeza kuwa bado hajachoka kuendelea kutumbua watumishi wanaowanyonya wananchi wanyonge, ambao wanakula rushwa bila huruma pamoja na mafisadi.

Alisema ataendelea na utaratibu huo. Rais Magufuli leo anaendelea na ziara yake mkoani humo kwa siku ya pili, ambapo atatembelea kiwanda cha chaki wilayani Maswa, ikiwemo kuweka jiwe la msingi barabara ya Maswa Mwigumbi, Shinyanga.

Awali katika mikutano yake mkoani humo, Rais Magufuli akiwa Busisi mkoani Mwanza, alisisitiza kutotoa msaada wa chakula kwa kaya zinazokabiliwa na tatizo la njaa nchini.

Aliwataka wananchi kuzitumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao yanayostahimili ukame, badala ya kutegemea msaada wa chakula kutoka serikalini.

Wakati huo huo, viongozi wa Wilaya ya Kongwa walitakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kulima mazao yanayostahili ukame ya mtama na muhogo ili kuondokana na njaa inayotaka kuanza kunyemelea wilaya hiyo.

Rugimbana alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa ziara wilayani humo, ambapo alizungumza na kada mbalimbali za viongozi ikiwamo kamati ya ulinzi na usalama, watendaji wa halmashauri, viongozi wa CCM na walimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Fadhili Nkurlu akizungumza na waandishi wa habari naye aliwataka wananchi wa wilaya yake kutunza chakula pamoja na kukitumia vizuri kiasi kidogo kilichopo na kuwataka wananchi kupanda mazao yanayostahimil ukame.

Jumanne, 10 Januari 2017

JESHI LA POLISI MKOA TANGA LIMEFANIKIWA KUWAOKOA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BOTI YA MV BURUDANI ILIOPATA AJALI KATIKA ENEO LA MWAMBA NYULI MKOANI HUMO.




Mwandishi wa habari Amina Omari akimpa pole mtoto Said Muhamed Said ambaye amepona katika ajali ya boti la MV Burudani ikitoka Tanga kwenda Pemba.


Baba mkubwa wa Said Muhamed Said akimtambua mtoto wake mmoja aliyepata ajali ya Boti  ya Mv Burudani iliyopata ajali usiku saa saba





Mtoto Cheupe akiwa amelazwa katika hospitali ya bombo kwa matibabu baada ya kunusulika katika ajali ya MV Burudani.







Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Godlack Mbwilu akieleza waandishi wa habari walivyo pokea majeruhi na maiti katika Hospitali hiyo kutokana na ajali ya Boti MV Burudan.
 

JESHI la polisi mkoa wa
Tanga limefanikiwa kwaokoa abiria wa boti ya 27 wa Boti ya Mv Burudani waliopata ajali usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani kutoka Tanga kuelekea Pemba

Ajali hiyo iliyosababishwa na dhuruba iliokipiga chombo hicho majira ya saa saba na nusu usiku katika eneo la mwamba nyuli uliopo mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Tanga Benadict Wakulyamba amesema wamepokea majeruhi 27 na maiti kumi na mbili (12) hadi saa nane mchana lakini jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la uokoaji  faya na bandari pamoja na wananchi bado wako kwenye eneo la tukio kaangalia kama wataweza kuokowa wengine waliobaki wakiwa hai au maiti.

Naye kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Godlack Mbwilu Amethibitisha kupokea majeruhi 25 wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya bombo na maiti 12  ikiwa ni watoto 6 na watu wazima ni 6 na mpaka saa nane mchana bado hawajatambuliwa.

kaimu mganga mfawidhi amewataka wananchi kujitokeza kutambua maiti zao
katika hospitali ya Bombo.








NA KWA TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YA SAUTI YETU WANATANGA