Jumanne, 28 Machi 2017

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AWAASA ASKARI KUACHA KUWABAMBIKIA WATU KESI.

Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.

Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.

Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema “ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA” endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.

Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.

Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.

Jumatatu, 20 Machi 2017

SIKU YA KINYWA NA MENO YAADHIMISHWA LEO WILAYANI TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobiass Milapwa akihutubia hadhala iliyofika katika maadhimisho ya siku ya kinywa na meno mkoani hapa hii leo  



Leo ni siku ya afya ya kinywa na meno kwa mkoa wa Tanga kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yamefanyika katika kiwanja cha Tangamano mgeni rasmi akiwa mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobiass Milapwa akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya katika Maadhimisho hayo.



Wanafunzi wa chuo cha afya ya kinywa na meno wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Tanga
Wadau na wanafunzi wakiwa katika maadhimisho ya afya ya kinywa na meno kiwanja cha Tangamano 






 

















JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA LAENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA WANAOFANYABIASHARA ZA MAGENDO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba akiwa katika doria ya kukamata bidhaa za Magendo kwenye Bandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza Mkoani Tanga, Picha ni mifuko ya sukari iliokuwa imefichwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba akiwa na Meneja  Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti mwenye shati la batiki pamoja na mashuhuda   katika doria ya kukamata bidhaa za Magendo kwenye Bandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza Mkoani Tanga, Picha ni wakikagua madumu ya mafuta yaliyo telekezwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba akiwa na OCD wa Pangani wakiefwatilia Jahazi la MV Yarazaki lililokuwa limebeba mali za magendo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba Meneja  Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti  pamoja  na OCD wa Pangani wakiwa kwenye doria ya kukamata bidhaa za Magendo kwenye Bandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba Meneja  Forodha wa TRA Mkoa wa Tanga Jumbe Magoti  wakikagua moja ya chombo kinachotumika kuingiza bidhaa za magendo kutoka nchi mbalimbali.

TANGA
JESHI la polisi mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na T.R.A  Uvuvi Doria alfajiri ya tarehe 19/3/2017 katika doria ya pamoja  kwenye bandari bubu ya kigombe kata ya Kigombe Wilayani Muheza Mkoani hapa wamefanikiwa kukamata Jahazi moja yenye namba za usajiri Z 1221 MV Yarazaki ambayo Nahodha na Mmiliki hajafanikiwa kikiwa na Shehena ya bidhaa za Magendo.

Akizitaja bidhaa ambazo zimekamatwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Benedict Wakulyamba amesema tumekamata (1) Mafuta ya kula aina ya oki dumu 304 za lita 20, kutoka Indonesia, (2) Sukari Mifuko 64 ya kutoka Blazil (3) Mchele mifuko 10 kutoka Pakistan.

Mpaka Muda mwandishi wa Tanga One  blog anaingia mtamboni thamani ya bidhaa hizo hazijafaamika gharama yake.

Kamanda Wakulyamba ametoa wito kwa wale wote wanaofanya biashara za magendo kuacha mara moja biashara hizo na  kufanyabiashara kwa mfumo raisi wa kulipa kodi kwa ustawi wa nchi yetu.

Pia kamanda amesema operesheni hizi ni endelevu katika bandari bubu zote na hata nchi kavu jeshi  la polisi mkoani Tanga halite mfumbia macho yeyote anaye vunja sheria ya nchi.