Jumatano, 8 Machi 2017

NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA TAMISEMI SULEMANI JAFO AWAPONGEZA UONGOZI WA WILAYA YA KOROGWE MKOANI TANGA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA SERIKALI.





NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo akiwasiri katika shule ya sekondari Mnyuzi wilayani korogwe vijijini na kusalimiana na Viongozi pamoja na Walimu. 
 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo akikagua vyumba vya madarasa katika shule ya mnyuzi wilayani korogwe mkoani Tanga hapa akimpongeza mkuu wa wilaya ya korogwe Mhandisi Robert Gabriel na mbunge wa korogwe vijijini Stevin Ngonyani kwa matumizi mazuri ya pesa za serikali.
 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo akikagua matundu ya vyoo vilivyojengwa kwakuzingatia watu wenye mahitaji maalumu (walemavu) katika shule ya sekondari mnyuzi korogwe vijijini.


Hili ni tundu moja la choo kwajili ya watu wenye mahitaji maalum ni kati ya matundu kumi ya vyoo kati yaliyojengwa katika shule ya Sekondari Mnyuzi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Hili ni moja ya tundu la choo cha kawaidi katika shule ya sekondari mnyuzi.




NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo akikagua Mabweni ya kulala Wanafunzi wa Shule ya sekondali Mnyuzi  Korogwe.



NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo  akimwangalia mkuu wa wilaya ya korogwe Mhandisi Robert Gabriel akijaribisha kupanda kitandani katika Mabweni ya kulala Wanafunzi  wa kike katika shule ya Sekondari Mnyuzi Korogwe vijijini.





Mbunge wa korogwe vijijini Stevin Ngonyani (Prof. Majimarefu) akitoa shukrani kwa Naibu waziri Jafo alipotembelea shule ya Mnyuzi iliyopo katika Jimbo lake.
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhandisi Robert Gabriel akimkaribisha NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo  ili azungumze na wanafunzi wa shule ya Mnyuzi iliyopo Korogwe vijijini.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika viwanja vya shule ya Sekondari Mnyuzi.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mnyuzi wilayani Korogwe wakimsikiliza NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za mikoa Tamisemi  Suleman Jafo ambaye hayupo kwenye picha wakati wa ziara yake shuleni hapo.
  









 


Jumanne, 7 Machi 2017

KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WANAWAKE WAJASILIAMALI WAKIWAJIBIKA.



Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, hawa ni wanawake wajasiliamali wakiwajibika katika soko la Msambiazi Wilayani Korogwe.



KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, wanawake mkoani Tanga wamejipanga kwa kufanya makongamano ya kupatiwa elimu ya kushiriki katika kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.

 Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii Jiji la Tanga Mwantumu Dosi wakati akifungua kongamano maalum yenye lengo la kuwajenga wanawake katika maswala ya uzalishaji mali na kuweza kupandisha thamani ya bizaa wanazozizalisha.

 Amesema katika kuiunga mkono serikali ili kuelekea uchumi wa viwanda ni vyema wanawake wakajiandaa kielimu kwa kuhakikisha watumia vyuo vya veta ili kujikita zaidi katika maswala ya kuzalisha bidhaa zenye tija na kujua masoko husika ya bidhaa wanazozalisha.

 Pia Dosi amewataka wananwake kujiunga katika vikundi ili jambo ambalo litasaidia kuwajengea uwezo hasa kwa kupata fursa mbalimbali iliwemo kupata mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yao.

,,Nawaomba wanawake wenzangu tujiunge kwenye vikundi kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kukopesheka kwani ni rahisi kujidhamini kuliko mtu mmojammoja hivyo tufanye hivi kwa kujiandaa na uchumi wa viwanda,,anabainisha Dosi.

Wakizungumza washiriki wa kongamano hilo wamesema changamoto kubwa inayowakabili wanawake kwa sasa ni mitaji pamoja na mfumo wa maisha ambao umetawaliwa na mfumo dume jambo ambalo linawarudisha nyuma wanawake wangi katika shughuli zao za uzalishaji mali.

Fatna Bendera yeye ni mmoja wa wanawake waliopata fursa ya kushiriki kongamano hilo ambaye anajishughulisha na uuzaji wa mbogamboga yeye anasema changamoto kubwa ni mitaji na kwamba wanawake wengi ni wajasiliamali wadogo hivyo wanashindwa kukidhi mashari ya taasisi zinazotoa mikopo.

Aidha wamemuomba rais Magufuli kutekeleza ahadi yake ya milioni hamsini kila kijiji ili waweze kukopa fedha hizo wanaamini kwamba zitawasaidia katika kukuza mitaji yao.
Wakizungumza na mwandishi wa Tanga one blog wanawake wa soko la Msambiazi wamesema kila wanapofanya biashara wanalipa ushuru lakini hawaoni mabadiliko yoyote katika soko hilo.

Asha Ramadhani ni mmoja ya wanawake wanaofanya biashara  katika soko  la Msambiazi lililopo wilayani Korogwe mkoani Tanga naye ameuomba uongozi wa soko hilo kuwasaidia kwani wanafanya biashara wakiwa juani na pia wateja hawaji kwa wingi kwani hata ukaaji wao katika soka hilo sio mzuri.

Naye Shabani Karimu mkazi wa Manundu Korogwe amesema soko la alhamisi la Msambiazi ni kubwa na linavutia hata yeye anatoka mjini kuja kufanya manunuzi ya wiki nzima katika soko hili kwa bei nafuu na vitu vizuri.

MWISHO





Jumatatu, 6 Machi 2017

JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA KWA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA ZA SERIKARI LAFANIKIWA KUKAMATA MAGENDO.

JESHI la polisi mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo zilizoingizwa kinyume cha utaratibu katika bandari bubu zilizopo mkoani humu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ukamataji wa bidhaa hizo kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Benadict Wakulyamba amesema wanefanikiwa kukamata mifuko ya 214 ya sukari, mifuko ya 138 ya mchele na madumu 132 ya mafuta katika bandari bubu zilizopo mkoani humu.

Pia jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 9 wakiwemo wanawake 2 na wanaume 7 kwa kosa la kukutwa na dawa za  kulevya aina ya mirungi, bangi na heroin.
Kamanda wakulyamba amesema wamefanya oparesheni  iliodumu kwa muda wa siku 7  lilifanikiwa kukamata bangi kg 300 ,mirungi kg 647 pamoja na heroin gram 39.

Hata hivyo jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Samsoni Karanga (36) aliyekuwa akitokea arusha kwenda mbeya akiwa na hati za kusafiria (Passport) 14 zenye majina tofauti za afrika ya kusini pamoja na hati 14 za homa ya manjano.

Kamanda amesema mtu huyo alikamatwa katika maeneo ya Mombo wilayani korogwe mtuhumiwa anashikiliwa na polisi wakati utaratibu wa kisheria ukiendelea ili afikishwe mahakamani.

Kamanda Wakulyamba ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano na kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na magendo pia kuwataka wananchi kuacha mara moja kwani kwa sasa magendo siyo biashara ya kufanya na kuwataka wakazi wa mkoa huu kufanya biashara za halali.

Kwa upande wake meneja wa TRA mkoa wa Tanga Swalehe Byarugaba amesema zoezi hili ni endelevu na wamejipanga kuhakikisha wanazuia bidhaa zinazo ingizwa kwa kukwepa kodi na hazina ubora na baadhi ya bidhaa hizo zimepita muda wake wa kutumika.

Pia Byarugaba amewataka watanzania wote kudhamini bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania.