Alhamisi, 3 Novemba 2016

VIJANA 150 WA MKOA WA TANGA WAPATIWA ELIMU YA UDEREVA WA BODABODA.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga David Mnyambugha akifunga mafunzo ya udereva kwa madereva wa bodaboda 150 walioitimu mafunzo yaliyo tolewa na chuo cha Fiucha Word Treing School katika ukumbi wa Polisi Mkoani Tanga na kuwataka vijana wa bodaboda kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wanao jihusisha na vitendo vya kiuhalifu.

Kaimu mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Mkoani Tanga Inspector Abel Kidayi wakati wa kufunga mafunzo katika ukumbi wa polisi Mkoa.
Mratibu wa mpango wa elimu kwa bodaboda Tanzania kutoka chuo cha Fiucha Word Treing School Pastory Patrick akitoa taarifa fupi ya mafunzo va udereva kwa mgeni Rasm Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.
 Wahitimu 150 waliopatiwa  mafunzo ya udereva wa bodaboda wakisikiliza kwa makini maelezo ya viongonzi mbalimbali waliohudhulia kwenye hafla ya kukabiziwa vyeti katika ukumbi wa Polisi Mkoa wa Tanga
Martha Mpelumbe afisa ugani  wa jiji la Tanga ni mmoja ya waliohitimu wa mafunzo ya udereva akipokea cheti chake na kuahidi kuwa dereva mzuri kwani kwa sasa anajua sheria za barabarani na   maana ya alama za barabarani.
Zuberi Kombo mmoja ya washiriki wa mafunzo ya udereva akipokea cheti kwa kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga David Mnyambugha.

 


JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LAWATUMBUA ASKARI WATATU.



JESHI la Polisi Mkoani Mwanza limewafukuza kazi askari watatu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu pamoja na upokeaji wa rushwa.

Akizungumza na askari hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema hatua imechukuliwa ili iwe fundisho kwa askari wengine wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Amesema askari mmoja kati ya hao amekutwa akiwa amelewa na kulala lindoni, huku wengine wawili wakituhumiwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda Msanga amesema ukiukwaji wa maadili ni chanzo cha ongezeko la uhalifu hivyo hatamvumilia askari yoyote atakaye kwenda kinyume kwa kufanya hivyo kunalichafulia hadhi jeshi la polisi kwa sababu ya makosa ya askari wachache.

Kamanda Msingi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha askari kufuata weledi wa kazi zao na kusema askari wanaotumia vyeo vyao kwa ajili ya kujipatia pesa kutoka kwa wananchi atawatumbua kabla kasi hiyo ya utumbuaji haijamfikia kwa kushindwa kuwasimamia.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU.



JESHI la Polisi nchini, katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika, limeendelea na operesheni za kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya usalama barabarani katika mikoa yote ili kudhibiti vitendo vya uhalifu na wahalifu. 

Katika operesheni hizo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha na katika baadhi ya mikoa, wananchi wameweza kusalimisha silaha kwa hiari katika vituo vya Polisi.

Operesheni hizi ni endelevu, na ili tuweze kufanikiwa zaidi katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususani katika kipindi hiki tunapoelekea mwisho wa mwaka, wananchi wanatakiwa kuwa makini na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu haraka kwa kutumia namba za bure 111 na 112 pindi wanapowatilia shaka watu wasiowajua katika maeneo yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Kwa wamiliki wa maduka makubwa, hoteli na maduka ya kufanyia miamala ya fedha kwa njia ya simu waangalie namna ya kuweka vifaa maalumu vyenye uwezo wa kurekodi mienendo ya watu wanaoingia na kutoka ama kufuata huduma katika maeneo yao ya biashara.

Pia, wananchi katika makazi yao waimarishe ulinzi kwa kutumia mpango wa ulinzi jirani kwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kubadilishana taarifa za hali ya usalama ili kuhakikisha mitaa yao inakuwa salama wakati wote.

Aidha, Jeshi la Polisi nchini linawataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu na kutii sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara. 

Jeshi la polisi nchini, litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, bila woga ama upendeleo katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Jumanne, 1 Novemba 2016

WATUMISHI 1663 WATUMBULIWA NA SERIKALI KWA KUZALISHA WATUMISHI HEWA.

WATUMISHI wa Umma 1,663 kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa wamechukuliwa hatua za kinidhamu baada ya kubainika kusababisha watumishi hewa 19,629 hadi Oktoba 25, 2016.
 
Waziri ya Nchi, Ofisi ya Rais, anayeshughulikia Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki amesema hayo jana Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mainda Hamad Abdallah (Mbunge wa Viti Maalum) alilohoji hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya watumishi waonarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
 
Akifafanua idadi hiyo, Waziri Kairuki alisema kuwa idadi ya watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu kutoka Wizara mbalimbali ni 16, Idara zinazijitegemea na Wakala za Serikali watumishi tisa, Sekretarieti za Mikoa watumishi sita na Mamlaka za Serikali za Mitaa watumishi 1,632.
 
Waziri Kairuki alisema kuwa watumishi hao wameisabishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 19, huku Halmashauri ya Kinondoni ikiwa na watumishi hewa 107 ambao waligharimu Serikali sh. bilioni 1.29, Kishapu watumishi 73 wamesababisha hasara ya kwa kugharimu sh. milioni 543 na kuonya kuwa waajiri waendelee kuchukua hatua za haraka na kudhibiti uwepo wa watumishi hewa ili kuipunguzia Serikali kuingia hasara kubwa badala ya kuwahudumia wananchi.  
 
Aidha, Waziri Kairuki alisema kuwa jumla ya watumishi 638 wamefunguliwa mashtaka polisi, watumishi 50 wanafanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na watumishi 975 mashtaka yao yamefikishwa kwenye Mamlaka zao za kinidhamu.

KIJANA ALIYEKAMATA NYOKA CHUMBAGENI TANGA




Kijana mwenye umri wa kati ya miaka 35 ambaye hakutaka jina lake litajwe mkazi wa chumbageni Tanga akiwaonyesha ushujaa kwa  amekamata nyoka katika eneo la chumbageni.