Ijumaa, 2 Septemba 2016

KIWANDA CHA SARUJI TANGA KIMEIPATIA SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA MIFUKO 400 YA SARUJI ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA UPUNGUFU NA UCHAKAVU WA VYUMBA VYA MADARASA.




 Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa mwalimu  mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.

Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.





Mkuu wa fedha kiwanda cha saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni Afisa Uhusiano , Nour Mtanga  na mkuu wa Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.


HABARI KAMILI
KIWANDA Cha Saruji Cha Simba  Cement  kilichopo Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Akizungumza katika wa halfa fupi ya makabidhiano , Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Malambugi alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii yakusaidia  elimu” alisema Malambugi.

Alimtaka mwalimu na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school,  Julias Shulla, alishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Shulla alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

Pia alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa  changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo  kwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.

BAADHI YA WANANCHI WALIOSHUHUDIA KUPATWA KWA JUA WAINGIWA NA HOFU YA KUPATA ULEMAVU WA MACHO.


WANANCHI   walioshuhudia   tukio la  kupatwa kwa  jua Rujewa  wilayani Mbarali mkoa Mbeya  hofu yatanda  kupatwa kwa  ulemavu  wa macho  kutokana na  kushuhudia   tukio  hilo pasipo  miwani .

 Wakizungumza na mtandao huu  wa matukiodaimaBlog wananchi hao wamelalamikia utaratibu mbovu wa serikali ya mkoa wa Mbeya kupitia idara  ya afya kushindwa kupeleka vifaa vya kutosha hasa  miwani ya kuwezesha kushuhudia jua bila madhara

Amos Sanga na Amina Kyando walisema pamoja na kukesha kusubiri tukio hilo ila wameondoka eneo hilo bila kuona tukio hilo kutokana na hofu ya kupatwa ulemavu wa macho

Hivyo walisema moja kati ya miradi ambayo serikali inapaswa kuanzishwa eneo hilo ni pamoja na kituo cha afya maalum kwa ajili ya kutibu macho kutokana na wananchi wengi kushuhudia tukio hilo bila kinga.

 Huku mamlaka ya hifadhi za Taifa (Tanapa) ikitumia tukio hilo kuanzisha lango maalum laUtalii kuingia hifadhi ya Taifa ya Ruaha lango la Ikoga na kutoa ofa  kwa wanafunzi zaidi ya 100 Kutembelea hifadhi hiyo bure

Akizungumza katika tukio hilo afisa habari wa Tanapa Paschal Sherutete alisema kuwa tukio hilo limefungua fursa kubwa kwa watanzania kuendelea kupenda utalii wa ndani pia wao Tanapa kama njia ya kutangaza utalii wameona ni vema kufungua lango hilo.

Sherutete alisema tukio hilo la kupatwa kwa jua limeonyesha jinsi ambavyo watanzania wanavyopenda utalii na kuwa idadi ya wananchi waliofika kwenye tukio hilo ni ishara tosha kuwa suala hilo linawezekana.

Hata hivyo aliwataka watanzania kuendelea kutembelea hifadhi za Taifa badala ya kuwaachia wageni pekee.

Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa chama cha waandishi wa habari za utalii na uwekezaji Tanzania ( Tataji)  Felix Mwakyembe  alisema kuwa tukio hilo limefungua utalii kwa mkoa wa Mbeya na Njombe na kuwa ni vema suala hilo kuendelezwa zaidi

Alisema kwa kuanza wao kama wanahabari wameanzisha chama cha utalii na uwekezaji hasa  kuona kanda ya nyanda za juu kusini inapaa katika utalii na uwekezaji

Hata hivyo alisema wao ndio wamehamasisha zaidi tukio hilo na kumekuwa na mafanikio makubwa zaidi kuwa na wageni toka nje wengi

kuwa kupitia tukio hilo baadhi ya watalii toka nje wamepanga kutembelea eneo la Ihefu ambako ni miongoni mwa vyanzo vya maji vya Mto Ruaha mkuu na kutembelea hifadhi ya Ruaha

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala akizungumza na wananchi hao waliofika kushuhudia tukio hilo japo alisema mkoa wa Mbeya kupitia tukio hilo wanampango wa kulienzi eneo hilo kwa kujenga mradi wa kumbukumbu

Mwanasayansi Dr Noorali Siwaji ambae ni mhadhiri wa chuo kikuu Huria cha Tanzania alisema tukio hilo ni kazi nzuri inayofanywa na Wanasayansi nchini

Japo alisema kuwa tukio hilo ni watu kujifunza sayansi na kuwa kupatwa huko kwa jua ni matukio ambayo hutokea Mara chache zaidi na kuwa wananchi wameshuhudia kupatwa kwa jua kwa mwonekano wa Pete.



Alhamisi, 1 Septemba 2016

MADALALI WA NHC WATOA VYOMBO VYA OFISI ZA GAZETI LA TANZANIA DAIMA.

Madalali wa NHC wamefika katika ofisi za gazeti la  Tanzania Daima asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa ofisini kutokana na deni la pango la mmiliki wa gazeti hilo, Freeman Mbowe.

Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amesema wako kwenye msukusuko mkubwa lakini wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida.