ASKARI mmoja wa Jeshi la Wananchi Tanga (JWTZ)
MT .69500 s/sgt John Komba pamoja na wakazi wengine watatu wa jijini Tanga wamefikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa kosa la kusababisha kifo cha
aliyekuwa kondakta wa daladala inayosafiri kati ya Nguvumali na Raskazoni,
Salim Kassimu (18) mkazi wa
Mwamboni.
Akisoma shitaka
la mauaji linalowakabili watuhumiwa hao na Wakili wa Serikali, Donata Kazungu mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hilda Lyatuu alisema mnamo Januari 26 mwaka huu katika kambi ya JWTZ iliyoko
kata ya Nguvumali jijini Tanga mshtakiwa Komba pamoja na wenzake watatu walimuua
Salim Kassim katika eneo la kambi hiyo.
Wakili Kazungu
aliwataja washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Adamu Juma (20), Sofia John
(20) ambao ni mwanafunzi, Yohana Warioba na Bernard Nicholaus ambao ni wanamgambo
wanaolinda katika kambi hiyo.
Hata hivyo,
watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutoka na mahakama hiyo kutokuwa na
mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Upelelezi kuhusu
kesi hiyo haujakamilika na hivyo itatajwa tena Februari 26 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni