Jumanne, 10 Januari 2017

JESHI LA POLISI MKOA TANGA LIMEFANIKIWA KUWAOKOA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BOTI YA MV BURUDANI ILIOPATA AJALI KATIKA ENEO LA MWAMBA NYULI MKOANI HUMO.




Mwandishi wa habari Amina Omari akimpa pole mtoto Said Muhamed Said ambaye amepona katika ajali ya boti la MV Burudani ikitoka Tanga kwenda Pemba.


Baba mkubwa wa Said Muhamed Said akimtambua mtoto wake mmoja aliyepata ajali ya Boti  ya Mv Burudani iliyopata ajali usiku saa saba





Mtoto Cheupe akiwa amelazwa katika hospitali ya bombo kwa matibabu baada ya kunusulika katika ajali ya MV Burudani.







Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Godlack Mbwilu akieleza waandishi wa habari walivyo pokea majeruhi na maiti katika Hospitali hiyo kutokana na ajali ya Boti MV Burudan.
 

JESHI la polisi mkoa wa
Tanga limefanikiwa kwaokoa abiria wa boti ya 27 wa Boti ya Mv Burudani waliopata ajali usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani kutoka Tanga kuelekea Pemba

Ajali hiyo iliyosababishwa na dhuruba iliokipiga chombo hicho majira ya saa saba na nusu usiku katika eneo la mwamba nyuli uliopo mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoani Tanga Benadict Wakulyamba amesema wamepokea majeruhi 27 na maiti kumi na mbili (12) hadi saa nane mchana lakini jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la uokoaji  faya na bandari pamoja na wananchi bado wako kwenye eneo la tukio kaangalia kama wataweza kuokowa wengine waliobaki wakiwa hai au maiti.

Naye kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo Dkt. Godlack Mbwilu Amethibitisha kupokea majeruhi 25 wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya bombo na maiti 12  ikiwa ni watoto 6 na watu wazima ni 6 na mpaka saa nane mchana bado hawajatambuliwa.

kaimu mganga mfawidhi amewataka wananchi kujitokeza kutambua maiti zao
katika hospitali ya Bombo.








NA KWA TAARIFA ZAIDI ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YA SAUTI YETU WANATANGA

Jumatatu, 9 Januari 2017

SILAHA YA KIVITA AINA YA SMG MALI YA HIFANZI YA SAADANI ILIYOKUWA IMEIBIWA NA ALIYEKUWA MFANYAKAZI YAKUTWA IMEFICHWA KICHAKANI.



SILAHA ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. 

Silaha hiyo inadaiwa iliibiwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini. 

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Bonaventura Mushongi amesema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka zamu ya lindo la geti hilo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo. 

“Huyu askari alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana zamu ya ulinzi hivyo alitoka na silaha yake akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi na ndipo ilipoibiwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi hiyo,” alisema. 

Mushongi alibainisha kuwa baada ya wizi huo, askari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) walianza msako na kupitia taarifa ya msamaria mwema walimkamata mtuhumiwa huyo, mkazi wa Tegeta Kibaoni ambaye alikwenda kuonyesha alipokuwa ameificha kichakani ikiwa na risasi 30. 

Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk James Wakibara alisema wameshtushwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea na kwamba, zaidi ni baada ya kukuta mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa mtumishi wao na aliacha kazi miezi kadhaa iliyopita yeye mwenyewe. 

Dk Wakibara alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano lilioutoa toka siku ilipoibiwa silaha hiyo hadi ilipopatikana.