Jumatatu, 6 Februari 2017

WAZIRI WA ARDHI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA MANYARA NA TANGA KUTOA ELIMU YA KUFANIKISHA ZOEZI LA KUPIMA MPAKA.



KIKAO cha utekelezaji wa uhakiki wa mpaka wa wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Kilindi mkoani Tanga kimefanyika  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga na kujumuisha viongozi mbalimbali kutoka katika mikoa yote miwili.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuliwa na waziri wa Adhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ambaye aliwaagiza viongozi wa wilaya husika kuwaelimisha wananchi wa maeneo hayo ili kufanya zoezi hilo la uhakika mipaka kuisha kwa wakati.

Waziri Lukuvi alisema mipaka huo wa kilindi na kiteto umeshaakikiwa kwa  mara mbili bado mgogoro unaendelea kwa kipindi cha muda mrefu na hii ni mara ya tatu na yamwisho serikali haita rudia tena kupima mpaka huu.

Lukuvi alisema serikali haianzishi mpaka mpya ila katika mpaka uliopimwa kipindi cha nyuma na kuwekewa alama za mapipa ambayo yaliliwa na kutu itawalazimu kufwatilia na kuweka alama za guzo kama za barabara zisizo haribika kilahisi. 
  
Hata hivyo Lukuvi alisema wizara itatoa wapima kutoka nje ya mikoa hiyo miwili  ili kujenga imani na wananchi  pia  wapima hao watatoa taarifa kwa viongozi na wananchi ili kujua maendeleo ya zoezi hilo.

Waziri  Lukuvi alisema gn 65 ya mwaka 61 ndiyo itakayo ongoza kwani mipaka hii ilisha pimwa na inaongozwa kwa mujibu wa mamalaka na mujibu wa kisheriaya nchi.

Waziri Lukuvi amewahakikishia wananchi wa mikoa miwili Tanga na Manyara kufanya kazi zao kwa amani na hakuna mwananchi atakaye bughudhiwa na zoezi hili la uhakiki litakapoanza . 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella alisema mkoa wa Tanga umeridhia na uamuzi uliotolewa na kikao hicho cha viongozi kutoka mikoa yote miwili pamoja na Waziri mwenye dhamana hivyo kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Shigella alisema wizara imelichukua hili kulifanyia kazi na wananchi watoe ushirikiano pale wapima watakapo fika mkoani ili mgogoro uweze kuisha na wananchi wa wilaya ya kilindi na kiteto kuisi kwa amani .

Naye mkuu wa mkoa wa Manyara Joely Bendela alimshukuru waziri Lukuvi kufanya maagizo ya waziri mkuu Kassim Majaliwa  kwa vitendo ili kuondoa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya Kilindi  na Kiteto.

Bendera alisema wananchi wanatakiwa kushiriki kikimilifu katika zoezi ili litakalo fanywa na wapima kutoka wizara ya Ardhi ilikuonye watanzania kuwa kilindi kuna amani na kiteto kuna amani hakuna ugomvi.

Pia amewataka viongozi kuwekea mkazo mpaka huo kwani kwa kufanya hivyo watamaliza mgogoro wa mpaka huo na amewataka viongozi kutokengeuka katika makubaliano ya kuhakikisha mgogoro wa mpaka unatokomea kabisa kwani watanzania wote ni ndugu.
mwisho
  

Alhamisi, 2 Februari 2017

ASKARI JWTZ AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUUWA.

ASKARI mmoja wa Jeshi la Wananchi Tanga (JWTZ) MT .69500 s/sgt John Komba pamoja na wakazi wengine watatu wa jijini Tanga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa kosa la kusababisha kifo cha aliyekuwa kondakta wa daladala inayosafiri kati ya Nguvumali na Raskazoni, Salim Kassimu (18) mkazi wa Mwamboni.

Akisoma shitaka la mauaji linalowakabili watuhumiwa hao na Wakili wa Serikali, Donata Kazungu mbele ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi, Hilda Lyatuu alisema mnamo Januari 26 mwaka huu katika kambi ya JWTZ iliyoko kata ya Nguvumali jijini Tanga mshtakiwa Komba pamoja na wenzake watatu walimuua Salim Kassim katika eneo la kambi hiyo.

Wakili Kazungu aliwataja washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Adamu Juma (20), Sofia John (20) ambao ni mwanafunzi, Yohana Warioba na Bernard Nicholaus ambao ni wanamgambo wanaolinda katika kambi hiyo.

Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutoka na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Upelelezi kuhusu kesi hiyo haujakamilika na hivyo itatajwa tena Februari 26 mwaka huu.