Jumatano, 14 Juni 2017

BUNGE LATOA AZIMIO LA KUITAKA SERIKALI ICHUKUE HATUA KALI KWA WAHUSIKA WOTE WA MIKATABA MIBOVU YA MADINI.

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.

"Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema Mkuchika.

Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.

Jumanne, 30 Mei 2017

WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI CHARLS MWIJAGHE AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA YA KITAIFA MKOANI TANGA.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijaghe akifungua maonyesho ya Biashara katika viwanja vya Mwahako Jiji na mkoa wa Tanga.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijaghe akikagua Banda la CRDB Bank katika maonyesho ya Biashara katika viwanja vya Mwahako Jiji na mkoa wa Tanga.
  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijaghe akikagua Banda la Bandari Tanga akipokelewa na meneja wa Bandari Percival Salama katika maonyesho ya Biashara katika viwanja vya Mwahako Jiji na mkoa wa Tanga.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijaghe akikagua Mabanda ya wamama wajasiliamali mbalimbali walioshiriki katika maonyesho ya Biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwahako Jiji na mkoa wa Tanga.
  Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daud Mayeji akimweleza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijaghe mikakati ya Jiji kuelekea Tanga ya viwanda.












 



 
















Ijumaa, 26 Mei 2017

SERIKALI YA TANZANIA NA UGANDA ZATILIANA SAINI MKATABA WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA.



Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Profesa Paramagamba Kabudi na Waziri wa Nishati wa Uganda Bi. Irene Muloni wakitia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Profesa Paramagamba Kabudi (kulia)na Waziri wa Nishati wa Uganda Bi. Irene Muloni (kushoto)wakionyesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania baada ya kutia saini.